Karibu

Nyakaho Mturi Mahemba photo
Bi. Nyakaho Mturi Mahemba
Mtendaji Mkuu

: mfuko.utamaduni@michezo.go.tz

: + (255) 655-884 148

Karibu katika tovuti hii ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania. Katika tovuti hii utapata taarifa kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko, njia za mawasiliano, mitandao yetu ya kijamii, taarifa na matukio mbalimbali yanayotokea katika Taasisi hii. Lengo ni kuhakikisha kuwa taarifa zote muhimu zinazohitajika zinapatikana katika tovuti hii ili kukuwezesha kuwa na uelewa mpana wa majukumu na huduma zitolewazo na Mfuko.

Majukumu ya Mfuko ni pamoja na kuanzisha, kukuza na kuendeleza kazi za Utamaduni na Sanaa ili ziwe na ubora wenye kukidhi mahitaji ya  soko la ndani na nje ya nchi.

Ni matumaini yangu kwamba tovuti hii itasaidia upatikanaji wa taarifa zote zinazohitajika katika kukuwezesha  kupata huduma inayoendana na mahitaji yako. Endapo hautapata taarifa unazohitaji, tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupitia namba zetu za simu, barua pepe, mitandao ya kijamii au kufika katika ofisi za  Mfuko zilizopo Jengo la Utumishi, Block A 8 Barabara ya Kivukoni, 11101 Kivukoni, Ilala, Dar es salaam 

Karibu sana katika tovuti hii ili uweze kuhudumiwa kwani kwa kufanya hivyo utaondokana na vikwazo mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli za Utamaduni au Sanaa  na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yetu.

Nyakaho Mturi Mahemba
AFISA MTENDAJI MKUU