Malengo ya Mfuko
Lengo kuu la Mfuko ni kuinua ubora wa kazi za Utamaduni na Sanaa ili ziweze kujiendesha kibiashara na kutengeneza ajira nchini. Aidha, malengo mahsusi ni
- Kutoa huduma za mikopo, ruzuku na dhamana kwa walengwa; na
- Kutoa mafunzo kwa walengwa ili wapate ujuzi wa kufanya kazi zao kwa weledi na kuongeza tija.