Sisi ni Nani

Mfuko wa Utamaduni ulianzishwa na Serikali mwaka 1998 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni kwa kushirikiana na Serikali ya Uswidi, aidha Mfuko huu ulisitisha shughuli zake mwaka 2013 baada ya Serikali ya Uswidi kujitoa katika ufadhili wa shughuli za Utamaduni.

Serikali kupitia iliyokuwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilihuisha Mfuko wa Utamaduni mwaka 2020 na kupanua majukumu yake hadi katika Sekta ya Sanaa kwa lengo la kutekeleza Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 inayoielekeza Serikali kuanzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa kwa ajili ya kuimarisha Sekta za Utamaduni na Sanaa.

Mfuko huu umeanzishwa kwa Sheria ya ujumuisho wa wadhamini (Trustees’ Incorporation Act) kama ilivyorejelewa mwaka 2002 (CAP. 318 R.E. 2002) na kupewa hati ya usajili yenye namba 1776 tarehe 30 Septemba, 2020.