Majukumu ya Mfuko

  1. Kuratibu upatikanaji na utunzaji wa rasilimali fedha ili kuwezesha ukuaji na uimarishaji wa sekta za Utamaduni na Sanaa nchini;  
  2. Kutoa mikopo na ruzuku kwa walengwa wa uzalishaji wa kazi za Utamaduni na Sanaa;
  3. Kutoa mafunzo kwa walengwa ili kuwawezesha kupata weledi wa kutumia mikopo au ruzuku zitolewazo na Mfuko kwa namna iliyokusudiwa na yenye kuleta tija kwao na katika Sekta;
  4. Kutekeleza maelekezo ya Sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997 kuhusu “kuanzisha mifuko na kodi maalum kwa ajili ya kugharamia uhifadhi na uendelezaji wa Utamaduni”;
  5. Kuratibu, kusimamia na kushiriki katika maonesho, matamasha, warsha,tuzo na vikao kazi ili kutoa elimu kwa umma kuhusu manufaa ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa;
  6. Kuhamasisha uzalishaji wa kazi za kiutamaduni na sanaa zenye ubora wa juu kwa lengo la kukuza Sekta za Utamaduni na Sanaa nchini; 
  7. Kuratibu mchakato wa upatikanaji wa wanufaika wa huduma za MFUKO; 
  8. Kuratibu upatikanaji wa vitendea kazi na uendelezaji wa miundombinu kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za MFUKO; 
  9. Kushirikiana kisekta na wadau wa kitaifa na kimataifa kwa ajili kuongeza ujuzi, kubadilishana uzoefu na kujenga mahusiano; na
  10. Kufanya tathmini na ufuatiliaji wa miradi na fedha za MFUKO.