WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO AFUNGUA WARSHA YA KUWAJENGEA UWEZO WADAU WA UTAMADUNI NA SANAA
- 15 August, 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Julai 27, 2023 amefunga warsha ya kuwajengea uwezo wadau wa Utamaduni na Sanaa, kuhusu Mikopo inayotolewa na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania kupitia Benki ya CRDB, iliyofanyika makao makuu ya Benki hiyo Palm Beach/Upanga Road Jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza wakati wa kufunga warsha hiyo Mhe. Chana amewataka wadau hao kuchangamkia fursa hiyo ili kuwawezesha kuandaa kazi bora za utamaduni na Sanaa ili kuendana na soko lililopo kwa sasa la kazi hizo.
Warsha hiyo imelenga kuwajengea uelewa juu ya namna ya kupata mkopo na faida zake katika kazi zao.
Warsha hiyo imeudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mh. Tale Tale (Babu Tale), Mkurugenzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania Ndugu Abdulmajid M Nsekela na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko Bi. Nyakaho Mahemba.