WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MHE. DKT. NDUMBARO ASISITIZA KUFANYA SANAA KIBIASHARA
- 25 October, 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ametoa wito kwa wadau wa Sekta ya Utamaduni na Sanaa nchini wafanye kazi kibiashara ili wafanye kazi zaidi na kutengeneza ajira nchini. Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema hayo Oktoba 12, 2023 jijini Dar es Salaam alipotembelea Ofisi za Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania
"Tubadilishe Sanaa kuwa biashara kupitia mikopo inayotolewa na Mfuko , Mfuko na Benki endesheni mafunzo juu ya elimu ya biashara kwa wasanii mara kwa mara ili wasanii waweze kuelewa juu ya kufanya biashara kibiashara. Pia wasanii tujirasimishe ili tuchangie pato la Taifa kupitia zawadi kwa maana fedha hizi za mikopo ni kodi za wananchi kwa sababu. mkilipa kodi kiwango cha pato la Taifa kitaongezeka na kiwango cha mkopo kitaongezeka pia" amesisitiza Mhe. Dkt. Ndumbaro
Aidha amemuagiza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Bi. Nyakaho Mahemba ahakikishe kuwa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa unakuwa chanzo kikubwa katika kukuza ukuaji wa Sekta ya Utamaduni na Sanaa.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la maonesho Bi. Cynthia Patrick Henjewele amesisitiza kujirasimisha kwa jambo linalosaidia katika uendeshaji wa sanaa kwa uhuru zaidi na kufungua njia na uhaminifu katika utendaji kazi wa msanii mmoja mmoja na nichanzo kikubwa kufungua njia ya kupata kazi ndani na nje ya nchi.