KIKAO BAINA YA BODI YA WADHAMINI YA MFUKO WA UTAMADUNI NA SANAA TANZANIA NA KATIBU MKUU MSIGWA
- 06 November, 2023

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa amefanya kikao na Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania Novemba 03, 2023 katika jengo la Benki ya CRDB Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kilichoendeshwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Mfuko Ndugu Abdulmajid M Nsekela kimelenga kujadili Ajenda kutoka katika kamati mbalimbali za Mfuko zilizowasilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko Bi. Nyakaho Mahemba zilizohusu utendaji na uendeshaji wa Mfuko.