MHE. Dr. PINDI CHANA ATEMBELEA OFISI ZA MFUKO WA UTAMADUNI NA SANAA

  • 11 May, 2023
  • Dodoma
  • 05:00PM - 06:00PM
MHE. Dr. PINDI CHANA ATEMBELEA OFISI ZA MFUKO WA UTAMADUNI NA SANAA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Februari 23, 2023 amefanya ziara katika Ofisi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mara ya kwanza tangu ateuliwe kuongoza wizara hiyo.

Mhe. Waziri Chana  aliambatana na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Pauline Gekul, Mkurugenzi  Idara ya Utamaduni Dkt. Emmanuel Temu na  Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma.

Hata hivyo Mhe. Waziri alipata nafasi ya kuzungumza na  baadhi ya Wadau wa Sekta hizo ambao  walinufaika  na mikopo iliyotolewa na Mfuko huo hivi karibuni.