Pongezi kwa uzalishaji wa maudhui ya kuelimisha jamii.

  • 23 July, 2026
  • African Liberation Heritage Center
  • 02:00PM - 03:00PM
Pongezi kwa uzalishaji wa maudhui ya kuelimisha jamii.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa amemkabidhi Mtengeneza maudhui Mtandaoni, Ndg.Abdul Chacha maarufu kama Headmaster fedha tasilimu shilingi Milioni tano, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika kuzalisha maudhui yanayoelimisha jamii.
Katika hafla hiyo Bw. Msigwa amehimiza vijana kushirikiana na kupeana fursa, akisisitiza kuwa serikali inaendelea kuwaunga mkono vijana wabunifu na kutaka vijana kutokubaniana na kupeana fursa.