Warsha ya Kuwajengea Uwezo Wadau wa Utamaduni na Sanaa Mkoa wa Mtwara

Mfuko wa Utamaduni na Sanaa nchini, umetoa mafunzo kwa wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya Mkoa wa Mtwara yanayolenga kuwajengea uwezo wa namna bora ya kuchukua mkopo na kurejesha kwa wakati kufuatia Serikali kutoa Bilioni 20 kwa mwaka wa fedha 2023/2024.