MAFUNZO YA URASIMISHAJI WA BIASHARA NA UJUZI
Washiriki wa Mafunzo ya Urasimishaji wa Biashara na Ujuzi wanaendelea kunufaika na mafunzo ya ususi wa vikapu yanayofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam. Mafunzo hayo yalianza rasmi siku ya Jumatatu tarehe 15/12/2025 yakiwa nalengo la kuwajengea uwezo wajasiriamali katika kuendeleza na kurasimisha shughuli zao za kiuchumi ili kuongeza thamani na ubora wa bidhaa zao.